WATAALAMU NA WASIMAMIZI WA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI YA TIKETI ZA VIVUKO TEMESA WAPATIWA MAFUNZO

Kampuni ya Maxcom Africa Limited imeanza kutoa mafunzo kwa wataalamu wa TEHAMA na wasimamizi wa mifumo ya kielektroniki ya kukatia tiketi katika vivuko vya Wakala wa Ufundi na Umeme nchini TEMESA. Mafunzo hayo ambayo yatachukua wiki mbili yanaratibiwa na kampuni ya Maxcom Africa Limited na yana lengo la kuhakikisha kwamba wataalamu hao wanajengewa uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo mara kwa mara zimekuwa zikijitokeza katika mifumo hiyo ya kielektroniki ya kukatia tiketi katika vivuko vya wakala