MTENDAJI MKUU TEMESA AFUNGA MAFUNZO IPSAS

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu mwishoni mwa wiki hii amewatunuku vyeti wahasibu wa wakala huo waliohitimu mafunzo ya Ufungaji wa Hesabu za Serikali kwa mfumo wa IPSAS. Mafunzo hayo yalichochukua muda wa siku tano yaliendeshwa na Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Ernst and Young katika ukumbi wa mikutano uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.