KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO

Wakazi wa jiji la Mwanza mapema leo wameshuhudia tukio la kushushwa kwenye maji kwa Kivuko kipya cha MV. Mwanza baada ya kufikia hatua za mwisho za kukamilika kwa ujenzi wake. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ametoa pongezi kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kusimamia mradi huo kwa mafanikio makubwa. Aidha, ameipongeza Kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Ltd ya jijini Mwanza kwa kujenga kivuko hicho kwa ubora wake.