TEMESA NA TARURA WATOA MAFUNZO KWA WATUMIAJI TAA ZA BARABARANI MOROGORO

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupitia kikosi cha Umeme kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara mijini na vijijini (TARURA) wametoa mafunzo kwa watumiaji wa taa za barabarani mkoa wa Morogoro, mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya mji na yalihusisha watembea kwa miguu, waendesha bodaboda,baiskeli, waendesha daladala za abiria pamoja na bajaji na yalilenga kuwajengea uelewa na jinsi ya kuzingatia alama za taa hizo za kisasa ambazo zilifungwa hivi karibuni katika Manispaa hiyo. Akitoa mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Kikosi cha Umeme Mhandisi Pongeza Semakuwa aliwataka watumiaji wa barabara hizo kuheshimu sheria na alama za barabara ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea, aliwakumbusha pia kuzitunza taa hizo kwakua zimeigharimu serikali fedha nyingi.