ZIARA YA KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA MIKOA YA LINDI, MTWARA NA RUVUMA

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amemaliza ziara yake mikoa ya kusini, mara hii akitembelea mkoa wa Lindi, Mtwara na Ruvuma ambapo pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi pia alipata fursa ya kukagua usalama wa vivuko vinavyotoa huduma katika maeneo hayo pamoja na karakana za mikoa hiyo.