MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WATENDAJI WAKE KUWEKA MAZINGIRA YA KUJITEGEMEA KWA KUZALISHA MAPATO ZAIDI.

Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watendaji wake katika vituo vyote vya TEMESA nchini kuanza kujenga mazingira ya kujitegemea na kuondokana na fikra za kutegemea fedha kutoka Serikalini.
Agizo hilo limetolewa na Mtendaji huyo alipotembelea karakana ya TEMESA iliyopo mkoani Geita na kujionea kazi zinazofanywa na karakana hiyo na kuagiza watendaji wake kutafuta mbinu mbadala ya kuzalisha mapato ili waweze kujiendesha wenyewe.

Read more...

TEMESA SHINYANGA YAZIDAI MILLIONI 163 HALMASHAURI, MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI

Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Shinyanga inazidai Halamashauri, Mashirika na Taasisi za Serikali mkoani humo jumla ya shillingi 163,269,269.82 kutokana na kupata huduma ya matengenezo ya magari.
Katika taarifa yake kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali amesema madeni hayo ni ya mwaka wa fedha 2016/2017 na wamesha wasilisha madai yao kwa wahusika na wanasubiri kulipwa.

Read more...