TEMESA SHINYANGA YAZIDAI MILLIONI 163 HALMASHAURI, MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI

Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Shinyanga inazidai Halamashauri, Mashirika na Taasisi za Serikali mkoani humo jumla ya shillingi 163,269,269.82 kutokana na kupata huduma ya matengenezo ya magari.
Katika taarifa yake kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali amesema madeni hayo ni ya mwaka wa fedha 2016/2017 na wamesha wasilisha madai yao kwa wahusika na wanasubiri kulipwa.


Mhandisi Riziki Lukali aliwataja wadaiwa hao kuwa ni TANROADS Shinyanga Sh 24,193,733.21, TANESCO Shinyanga Sh Milioni 96,267,987.63, DED Kishapu Sh 6,753,735.03, RAS Shinyanga Sh 2,742,097.36, KUWASA Kahama Sh 9,855,714, KASHUWASA Shinyanga Sh 1,992,430, TBA Shinyanga Sh 5,103,062.56, Mahakama Kuu Shinyanga Sh 5,470,628.91, Uhamiaji Shinyanga Sh 896,333.63, DAS Kishapu Sh 1,071,573.57, NSSF Shinyanga Sh3,798,184 pamoja na RMO Shinyanga shilingi 5,123, 789.92 milioni na jumla ya madeni hayo yote ni Sh 163,269,269.82.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amefurahishwa na utaratibu wa TEMESA Shinyanga wa kuzuia magari ya taasisi, halmashauri na mashirika yanayodaiwa na kituo hadi hapo yatakapolipiwa gharama za matengenezo.


Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha Shinyanga alipotembelea kituoni hapo katika ziara yake katika vituo .


Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (menye shati la rangi ya bluu)akiangalia gari la TANESCO Shinyanga, linaloshikiliwa na TEMESA Shinyanga kwa sababu ya deni la Sh Millioni 96 kushoto ni Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali