MV. MWANZA

News Image

Posted On: July 11, 2018


Kivuko Kipya cha MV. Mwanza leo kimefanyiwa majaribio kwa muda wa saa nne majini kabla ya kuanza kutoa huduma katika eneo la Kigongo na Busisi jijini Mwanza.

Kivuko hiki kimejengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza, kimegharimu jumla ya tshs 8.9 bilioni fedha kutoka vyanzo vya ndani vya Serikali. Kinauwezo wa kubeba tani 250 sawa na abiria 1000 na magari 36 kwa wakati mmoja