Nane Nane 2018 Nyakabindi

News Image

Posted On: August 02, 2018


Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) unashiriki maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu.

Ufikapo katika banda la TEMESA utapata huduma ya

1. kupimiwa gari bure kwa kutumia kifaa cha kielektroniki cha kubaini magonjwa ya magari

2. Maelezo ya namna sahihi ya kutumia taa za barabarani

3. Kujifunza matumizi salama ya vivuko na ukodishaji wa mitambo ya serikali inayosimamiwa na TEMESA

4. Huduma za ushauri katika nyanja za uhandisi mitambo, elektroniki, na viyoyozi