SABASABA

News Image

Posted On: July 06, 2018

Wakala wa Ufundi na Umeme na TEMESA unawakaribisha Watanzania wote kutembelea Banda letu kwenye Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere maarufu kama Sabasaba kuanzia June28 hadi July 13 2018.
Banda la TEMESA linapatikana nyuma ya mabanda ya BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Kwenye banda la TEMESA utapata fursa ya kufahamu kuhusu
i. Kufanya matengenezo ya Magari, pikipiki na Mitambo ya Serikali katika Karakana ambazo zipo kila Mkoa;

ii. Kufanya matengenezo na Usimikaji wa Mifumo ya Umeme, Mabarafu, viyoyozi na Elektroniki;

iii. Kufanya matengenezo ya taa za kuongozea magari (Traffic Signals) na taa za barabarani (Street Lights);

iv. Kukodisha magari kwa ajili ya usafiri wa Viongozi (VIP Vehicles) yaliyopo katika Kitengo cha GTA (Government Transport Agency;

v. Kukodisha mitambo ya kuzalisha kokoto, na mitambo ya kazi za barabara;

vi. Uendeshaji wa Vivuko vya Serikali;

vii. Kutoa ushauri wa Kitaalamu kwa Serikali na Umma kwa ujumla katika nyanja za uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki;

viii. Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu usimikaji wa mifumo mipya ya uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki; na

ix. Kufanya usanifu na Usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi wa Ufundi Umeme na Elektroniki ili kukidhi viwango vinavyotakiwa na kwa kulingana na matakwa ya Sheria na Taratibu zinazoongoza taaluma husika.