TEMESA YAALIKA WADAU KUJADILI RASIMU YA MUONGOZO WA MATENGENEZO YA MAGARI

News Image

Posted On: March 21, 2019

Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) umealika wadau kutoka taasisi mbali mbali za Umma na binafsi nchini kujadili Rasimu ya Muongozo wa Matengenezo ya magari, pikipiki, mitambo, usimikaji na matengenezo ya mifumo ya umeme, elektroniki, viyoyozi, majokofu, kangavuke pamoja na ushauri wa kiufundi. Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wazabuni, wamiliki wa gereji teule, maafisa usafirishaji na wadau kutoka taasisi za Umma na binafsi walioko mkoa wa Dar es Salaam kilifanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko Dar es Salaam ambapo kilifunguliwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Maselle.