Equipment Hire

1.0 KITENGO CHA UKODISHAJI MITAMBO

Lengo:

1. Kutengeneza mitambo ya Serikali na kuirejeshea uwezo wa kufanya kazi na kuikodisha.

2. Kuinua kipato na kuwajengea uwezo wakandarasi wadogowadogo hasa wazawa kwa kukodisha mitambo ya Serikali ili kuwapa uwezo kutekeleza miradi ya serikali iliyolenga.

3. Kusaidia na kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya serikali kutokana na upatikanaji wa mitambo yenye masharti rahisi na bei nafuu.

4. Kutoa huduma za ukodishaji magari madogo kwa Wizara na taasisi za Serikali kwa ajili ya viongozi na yadi za GTA.


2.0 MIKOA NA VITUO VINAVYOTOA HUDUMA ZA UKODISHAJI NA USIMAMIZI

Mikoa inyotoa huduma ya ukodishaji ni kama ifuatavyo:

Arusha Dodoma Geita

Kagera Katavi Kigoma

Lindi Manyara Mbeya

Morogoro Mtwara Mwanza

Njombe Pwani Rukwa

Simiyu Shinyanga Tabora

Tanga Kituo cha GTA Iringa


3.0 MIPANGO YA KITENGO ILIYOPO KWA SASA

1. Kununua mitambo mipya kutokana na fedha za ndani zinazochangiwa sehemu ya mapato ya sasa (40%) makusanyo.

2. Kuuza mitambo yote iliyochakaa na ile iliyopitwa na wakati (Outdated Models) ili kuchangia kupata mitambo ya kisasa.